Bifu la Diddy na 50 Cent ladaiwa chanzo wivu wa mapenzi

Bifu la Diddy na 50 Cent ladaiwa chanzo wivu wa mapenzi

Baada ya mkali wa Hip-Hop kutoka nchini Marekani Diddy, na 50 Cent kutokuwa na maelewano mazuri kwa kipindi cha muda mrefu hatimaye imedaiwa kuwa bifu la wawili hao limetokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizofikishwa mahakamani na Rodney Jones, producer wa Combs, zimeeleza kuwa Diddy alikuwa akimlipa mzazi mwenza wa Cent aitwaye Daphne kwa ajili ya kutoa huduma za ngono.

Aidha kufuatiwa na sakata la msako wa Diddy, ‘rapa’ Cent amekuwa akikomenti kwenye posti mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii akionesha kufurahishwa huku akitoa maneno ya kejeri kutokana na anayoyapitia Diddy.

Ikumbukwe kuwa makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami siku ya Jumatatu, Machi 25, yamefanyiwa upekuzi na Mawakala ya Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.

Aidha mpaka kufikia sasa bado haijabainishwa ni wapi msanii huyo yupo huku watoto wake wawili wakiume waliokuwa wakishikiliwa na polisi #Justin na King Combs, wakiondoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi baada ya kuachiwa huru.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags