Biashara zenye faida ambazo watu huzidharau

Biashara zenye faida ambazo watu huzidharau

Haya haya kama kauli mbiu yetu inavyosema hakuna kukaa kilelemama ni kufanya biashara tu, hakuna kumuogopa mtu wala kiumbe yoyote kukukatisha tamaa, sasa week hii tumekusogezea mada ambayo nimuendelezo tu wa yale yale tuliokuwa tunayazungumza kuhusiana na biashara ambazo utazifanya ukapata faida licha ya watu kukudharau.

Je unatafuta biashara unazoweza kuzianzisha ukiwa na mtaji mdogo?

 Makala hii itakuonyesha biashara 6 ambazo unaweza kuanzisha mara moja kwa mtaji mdogo.

Kinachotakiwa kabla haujachagua biashara ya kufanya kazi kwa bidii, ukakamavu na kujiamani pia usisahau kujitoa siku zote biashara ni kujitoa. Yafuatayo ni baadhi ya mawazo ya kibiashara kwa watu wenye kipato cha chini nchini wale wenzangu na mie.

  • Biashara ya mitumba

Hii ni biashara ya mtaji mdogo unayoweza kuianzisha. Vijana wengi wamewekeza katika biashara hii na wanaendesha maisha yao yote kupitia uuzaji wa mitumba.

Unaweza kuuza nguo za mitumba kwa wafanyakazi wenzako na marafiki. Unachohitaji ni kujua aina ya mavazi wanayopenda wateja wako wa mara kwa mara na kisha uwafikishie. Baada ya kipindi fulani, utakuwa umechuma mtaji wa kutosha kwa minajili ya kupanua biashara yako na hata kufungua duka katika eneo zuri.

  • Kuuza mikoba ya wanawake

Hii ni biashara ambayo imeshamiri kwani wanawake wengi wanapenda sana mitindo. Unaweza kuanza kuiuza mikoba kwa kuanza na mkoba mmoja tu hii. Unaweza kununua mikoba hii kwa bei ya chini na kuiuza kwa bei ya juu.

Sio lazima ununue mikoba mipya, unaweza kuanza kwa kununua toka kwa wale wanaofanya biashara ya mikoba ya mitumba. Iwapo una kurasa za mitandao ya kijamii kama Facebook au Instagram, unaweza kuwa ukipost picha na hivyo kujihakikishia mauzo kutokana na wafuasi wako.

Hii ni biashara ambayo unaweza kufanya hata kama umeajiriwa.  Unahitajika tu kubeba mikoba michache kwenda nayo kazini na unaweza kuwauzia wafanyakazi wenzako. Sie wafanyabiashara tunasema biashara kokote bwana.

  • Kuuza matunda (fruits) na juice ya matunda

Hii ni njia nyingine yenye faida kubwa ya biashara ambayo inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa sana, Unahitaji tu kuwa na mashine ya kusaga na kuchanganya matunda ili iweze kuwa juice, cha muhimu ni kuwa msafi na bidhaa zako.

Nunua matunda yako menya vizuri, katakata matunda weka katika vifungashio vyake halafu weka katika fridge ili yaweze kupata baridi, katika muda wa lunch kimbia mara moja kachukue bidhaa zako, njoo uwauzie wafanyakazi wenzako.

Ili kupunguza gharama yako hata zaidi, unaweza kupanda mwenyewe baadhi ya matunda. Huhitajiki kuwa na shamba ili kuanza unaweza kutafuta magunia machache na kuyajaza udongo. Kisha, panda matunda kama vile passion na tikiti maji. Unaweza pia kuongeza mboga nyingine kama vile spinachi na kabichi. Mboga hizi zinaweza kuleta mapato ya ziada, hasa ikiwa unauza katika maeneo ya mijini.

  • Kuuza mayai

Hii ni moja ya biashara maarufu sana mtaani Hii ni biashara ambayo haihitaji muda wako mwingi sana. Unaweza kuanza kwa kuuza tray moja ya mayai au hata kama ni mbili taratibu watu watazoea na biashara kuwa kubwa. Ukiwa na akaunti mtandaoni itakuwa vizuri zaidi kwa ajili ya kutangaza biashara yako kwa wafuasi wako.

Hata hivyo, unahitaji kutenga mahali maalumu ambapo panaweza kuwa ndo office yake mfano unaweza kukodisha frem nakuhakikishia utashuhudia biashara yako ikikua bila mchango wa ziada.

Mfano siku hizi kuna watu tele wamefanya ubunifu wa kuuza mayai ya kuchemsha katika vituo vya magari (stendi), na ni ya moto muda wote, ubunifu waliotumia ni kuunganisha jiko kwa chini ili mayai yaweze kuwa ya moto muda wote. Uliza wanafanyaje na wewe uelekezwe uache kukaa nyumbani.

 

  • Kuuza maziwa

Hii ni biashara ambayo inafaida sana sana asikwambie mtu wallah, watu wengi siku hizi hawapendi kunywa maziwa kutoka katika makampuni ya kutengenezea vyakula, bali watu wengi hupendelea zaidi maziwa fresh yale yenyewe yanayotokea kwenye ng’ombe na sio haya ya mchongo.

Na hii biashara unaweza kuifanya katika mazingira yoyote mfano kama katika stendi za magari, mashule, vyuoni, na sehemu ambazo zinamkusanyiko wa watu wengi kama vile Kariakoo ama Karume na itapendeza zaidi maziwa ukayauza na vitafunio na inabidi uwe na maziwa mchanganyiko kama vile freshi, mtindi, yenye viungo nk.

 

  • Kuuza chakula katika maeneo ya ujenzi

Uuuuuwiiii! Sijui niielezeaje hii biashara maana ina zaidi ya faida. Kuna mama mmoja nimemshuhudia akijenga na kuboresha maisha yake kupitia biashara hii ya kuuza chakula katika sehemu za ujenzi.

Ni bayana kuwa hii ni biashara ambayo una uhakika wa faida. Kile unahitaji kufanya ni kuandaa vyakula na kupeleka katika maeneo ya ujenzi, kama unavyojua ujenzi wa ghorofa au barabara hauishi siku moja unaweza kutumia hadi mwezi. Embu nambie mwenzi mzima au miezi miwili uwe unapeleka chakula bado hujafanikiwa tuu.

Cha muhimu cha kuzingatia kikubwa ni kuwauliza wale wajenzi leo wanapendelea kula ni haswa haswa, sio unapika wali wako kumbe wengine siku hiyo hawajiskii kula wali fanya kile ambacho wateja wako wanataka.

Amkeni amkenii haya haya mawazo ya biashara ndo hayo na nitaendelea kuwapatia kila siku mpaka mchoke nyie, karne hii sya sasa sio ya watu kubweteka tuu na kusubiri mwanaume ndo akuletee, weye mwanamama wewe kijana changamka siku hizi hakuna hizi kazi ya kiume au ya kike tunacho angalia ni mkono kwenda kinywani.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags