Biashara ya uwakala haitaki mbwembwe

Biashara ya uwakala haitaki mbwembwe

 

Niwasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano Tanzania, basi wote tusema kazi iendelee, kama kawaida ili mkono uende kinywani lazima kazi na juhudi ifanyike, katika juhudi hizo siyo vibaya ukijikita kwenye biashara ya uwakala wa fedha kupitia mitandao ya simu na benki.

Biashara ya uwakala imekuwa ikiendeshwa na watu wengi jijini Dar es Salaam na mikoa mingine lakini jambo ambalo linawafanya wengi washindwe kuendesha biashara hiyo ni kutokana na kudanganywa kuwa ina hasara sana.

Kwanza kabisa fahamu hakuna biashara isiyo na hasara lakini ni kulingana na vile wewe unavyoifanya. Kutoka na mitazamo hiyo Mwananchi Scoop tumeangazia namna ambavyo biashara hiyo inaweza kukutoa kimaisha na kukufelisha pia. Unachotakiwa kujua ni kwamba biashara ya uwakala haiitaji mbwembwe bali inahitaji vitu hivi;

  • Location

Kama nilivyo waambia hapo juu biashara ya uwakala haitaki mambo mengi, Inahitaji uifanya sehemu yenye mzunguko wa watu wengi.

Biashara hii unalipwa kulingana na miamala unayoifanya kwa mwezi so ukipata location yenye mwingiliano wa watu itakusaidia kufanya kazi kila siku na kuingiza hata zaidi ya laki moja kwa siku.

  • Mwonekano mzuri

Ili uwe mjanja katika biashara hii unatakiwa kuboresha mwonekano wa sehemu unayofanyia biashara mfano banda lako liwekee mwonekano ambao utamshawishi mteja kusogea ili aweze kupata huduma yako. Kwa sababu baadhi ya wateja wanachagua sehemu ya kuweka au kutuma pesa kutokana na mwonekano. 

  • Usalama

Kama unahitaji kufanya biashara hii, moja ya kitu unachotakiwa kuwa nacho makini ni usalama wa sehemu husika utakayofanyia kazi kuanzia wewe mwenyewe kuwa mkweli na hata mazingira biashara yako ilipo.

Mbali na kuhakikisha sehemu unayofanyia biashara zako iko salama pia unatakiwa kuwa makini na wateja watakao kuja kwani baadhi yao wapo kwa lengo la kutaka kukuibia.

Hivi ndiyo vitu vitatu muhimu ambavyo ni msingi mkuu wa kuendesha biashara ya uwakala, mambo mengine ya kuzingatia ni pamoja na muda wa kufunga, kuwa makini katika kutuma pesa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags