Beyonce amkataa Kamala na Trump

Beyonce amkataa Kamala na Trump

Mwanamuziki wa Marekani Beyonce ameripotiwa kuwakacha wagombea Urais nchini humo Kamala Harris na Donald Trump.

Haya yamejiri baada ya timu ya msanii huyo ikiwakilishwa na msemaji Yvette Noel Schure kukanusha tetesi zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa Beyonce yupo Chicago kwa akili la kutumbuiza kwenye mkutano Mkuu wa chama cha Democratic (DNC) ambao ni maalumu kwa ajili ya uteuzi wa Kamala Harris kugombea urais wa Marekani.

Hata hivyo Beyonce alikuwa na mpango wa kumshitaki Donald Trump kwa kutumia wimbo wake wa mwaka 2016 uitwao ‘Freedom’ bila ridhaa yake.

Kupitia video iliyochapishwa na mmoja wa watu wa Trump aliyetambulika kwa jina la Steve Cheung ilimuonesha mgombea huyo wa Urais akishuka kwenye ndege huku akicheza wimbo huo wa Freedom jambo ambalo lilifanya mashabiki kumtaka msanii huyo amchukulie hatua za kisheria.

Hata hivyo muda mchache baadaye video hiyo ilifutwa kwenye mtandao huo baada ya Beyonce kutaka kumshitaki Trump.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags