Benzema: Nimeamia Saudi Arabia kwasababu ni nchi ya kiislamu

Benzema: Nimeamia Saudi Arabia kwasababu ni nchi ya kiislamu

Aliekuwa mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema sasa anasema  sababu ya yeye kujiunga na klabu ya Al Ittihad ni kwakua nchi hiyo imejaa idadi kubwa ya waislamu.

Benzema mwenye umri wa miaka 35 ni Mwislamu mwenye imani thabiti, na alikamilisha uhamisho wake kutoka Real Madrid kwenda Al Ittihad Jumanne baada ya kupokea ofa nono.

Akizungumza kabla ya hapo na vyombo vya habari vya klabu ya Al Ittihad, alipoulizwa kwanini Al Ittihad, mshambuliaji huyo alijibu

 “Kwa sababu ni moja ya vilabu bora nchini Saudi Arabia, Ni klabu ambayo inaona shauku kubwa kutoka kwa mashabiki na ina mataji mengi” amesema Benzama

Benzema alitambulishwa kwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa Al Ittihad siku ya Alhamisi katika Uwanja wa King Abdullah Sports City na walihudhuria Zaidi ya mashabiki 60,000 katika hafla hiyo.

“Kwa sababu mimi ni Mwislamu na hii ni nchi ya Kiislamu, na daima nimekuwa nikitaka kuishi hapa, ni tofauti na Ulaya ninajisikia vizuri kuhusu hilo. Jambo muhimu zaidi, ni nchi ya Kiislamu. Ningependa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha, ni muhimu kwangu," Benzema alijibu alipoulizwa kwanini Saudi Arabia






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post