Benki ya dunia yaikopesha Tanzania billion 700

Benki ya dunia yaikopesha Tanzania billion 700

Nchi ya Tanzania imepata Mkopo wa Dola za Marekani Milioni 300 ambapo ni takribani billion 700 kwa pesa za kitanzani kwa ajili ya kuchochea uzalishaji, kuimarisha sekta ya kilimo na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Miongoni mwa yatakayotekelezwa ni pamoja na kuboresha utoaji wa huduma katika utafiti, ugani na mbegu, kuendeleza miundombinu ya kilimo vijijini pamoja na kuimarisha usimamizi wa Rasilimali Fedha na Uwekezaji.

Aidha mkopo huo umetolewa chini ya Programu ya matokeo ya (PforR) inayofadhiliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) na unalenga kusaidia utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post