Barabara ya mwendokasi yafungwa kuhofia bomu, Uganda

Barabara ya mwendokasi yafungwa kuhofia bomu, Uganda

Polisi nchini Uganda walifunga kwa muda mfupi barabara ya mwendokasi yenye shughuli nyingi zinazounganisha mji mkuu wa Kampala na uwanja wa ndege wa nchi hiyo baada ya hofu ya usalama, siku ya leo Jumatano.

Kikosi cha mabomu kilitumwa kufanya uchunguzi pembezoni mwa barabara kuu ya Entebbe kabla ya kuondolewa kwa kusimamishwa kwa matumizi ya umma, kulingana na ujumbe wa tweeter wa polisi.

Zoezi hilo lilifanikiuwa baada ya wenye magari kuelekezwa kwenye barabara ya zamani inayopita karibu na barabara ya mwendokasi hadi uchunguzi ukamilike na utaratibu wa kawaida wa trafiki kurejeshwa.

Ikumbukwe tuu barabara ya mwendokasi inayofadhiliwa na China ilifunguliwa mnamo mwaka 2018, pia ni barabara ya kwanza kabisa ya utozaji ushuru nchini humo.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags