Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezifungia Bar za wazi zaidi ya 80 ikiwemo Elements, Wavuvi Camp, Boardroom, Kitambaa Cheupe, Liquid, Warehouse na Soweto za Dar es salaam pamoja na Chako ni Chako, Rainbow, Gentleman za Dodoma na Kasiki ya Mwanza baada kukuta kelele zilizo kinyume cha sheria ya usimamizi wa mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na kanuni ya viwango vya udhibiti wa kelele na mtetemo ya mwaka 2015.
Akiongea wakati wa Mkutano na Wadau wa Mazingira Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema sheria hiyo imesema maeneo ambayo yanazunguka maeneo ya watu na kuna biashara kelele zinatakiwa kuwa 60 DBA wakati wa mchana na 40 usiku na kwamba sio mara ya kwanza kuwaonya ambao wamefungiwa “Wengine tuliwapa faini lakini waliendelea kukaidi, tumefungia Baa 19 Kindondoni, Ilala 25, Kigamboni 22, Temeke 12, Baa 5, Mwanza 6”
“Baadhi ya wale sugu ambao tumeshughulika nao tangu mwanzo na mpaka sasa wanaendelea kutusumbua, kuna Boardroom wa Wilaya ya Kinondoni, kuna Wavuvi Camp, Warehouse, Kitambaa Cheupe, Elements, Soweto, Liquid , kule Dodoma kuna Chako ni Chako, Rainbow, Gentleman, kule Mwanza kuna Kasiki”
“Hawa tumechukua hatua hizo za kufunga kwasababu sio mara ya kwanza kuwaonya tulishapita mara nyingi lakini hawakusikia, baada ya kuwafungia wengi wamefika kuomba msamaha na wengine wameomba wafunguliwe” amesema Dkt Gwamaka
Leave a Reply