Banda afunguka kuachana na  mdogo wa Kiba

Banda afunguka kuachana na mdogo wa Kiba

Baada ya maswali mengi juu ya ndoa ya beki wa klabu ya Richards Bay inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini, Mtanzania Abdi Banda, mwenyewe kajitokeza na kufafanua ilivyokuwa.

Staa huyu amethibitisha kuachana na mkewe wa kwanza, Zabibu Kiba ikiwa ni moja ya swali linaloulizwa na mashabiki wengi hususani mitandaoni, baada ya kuona picha za harusi yake mpya.

Banda ameeleza kwamba alichana na Zabibu tangu mwanzoni mwa mwaka jana ingawa hakusema sababu za kuvunjika kwa ndoa yao.

"Harusi yangu ilikuwa Jumamosi ya Mei, 18, 2024 kwenye msikiti wa Kichangani, Dar es salaam. Mke wangu anaitwa Bi Maryam ni Mtanzania mwenye asili ya Tanga. (Ndoa) haikuhudhuriwa na mastaa kwa sababu walikuwa na majukumu yao ya kikazi ila walinisapoti sana," amesema mchezaji huyo.

"Kuhusu binti yangu niliyezaa na mke wangu wa zamani Zabibu, anaishi na mama yake, kwani bado mdogo nikisema nimchukue atakuwa mnyonge, kwani kazi zangu haziniruhusu kukaa muda mwingi nyumbani."

Alipoulizwa kuachana na Zabibu itakuwa mwisho wako wa kushabikia muziki wa Ali Kiba? Banda amejibu, "nilikuwa shabiki wa Ali Kiba kabla sijamuoa dada yake, hivyo nitaendelea kushabikia kazi zake, kwani anaimba muziki mzuri."

Pia amejibu tetesi za chanzo cha kuachana na Zabibu zilizokuwa zinasemwa kwamba ilitokana na umbali, lakini Banda amesema: "Hiyo siyo sababu, niliishi nao muda mwingi, kikubwa hapo kila mtu ana amani, hivyo siwezi kuweka kila kitu mitandaoni."






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags