Baby Shark Dance ndiyo wimbo unaongoza kwa watazamaji YouTube

Baby Shark Dance ndiyo wimbo unaongoza kwa watazamaji YouTube

Katika enzi hizi za kidijitali ambazo mitandao ya kijamii na majukwaa ya video yanachangia kwa kiasi kuburudisha jamii na kufurahia muziki, wimbo wa watoto "Baby Shark Dance" kutoka kwa 'Pinkfong Kids' Songs & Stories umeonekana kuvutia mamilioni ya watu duniani. Ambapi kwa mwaka 2024, video ya wimbo huo inashikilia rekodi ya kuwa na watazamaji wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube.

Wimbo wa "Baby Shark" ulichapisha kwenye mtandao huo tarehe 17 Juni 2016 na hadi saa una zaidi ya watazamaji bilioni 14. Wimbo huo ni sehemu ya nyimbo za watoto kutoka Pinkfong, kampuni maarufu ya elimu inayojulikana kwa maudhui yake ya kufundisha na kuburudisha.

Kati ya vitu vinavyovutia kutoka kwenye wimbo huo ni video zake yenye picha za rangi angavu na rahisi kueleweka kwa watoto jambo lililopelekea kupata umaarufu zaidi duniani kote. Mbali na watoto pia wimbo huu umekuwa ukivutia hadi watu wazima.

Kutokana na idadi hiyo kubwa ya watazamaji katika wimbo huo ni wazi kuwa umekuwa kivutio cha kipekee kwenye mtandao wa YouTube. 'Baby Shark Dance' si tu wimbo maarufu bali pia ni sehemu muhimu ya historia ya YouTube, ikiwakilisha jinsi burudani na teknolojia vinavyoweza kuungana kwa njia ya kipekee.

Mbali na huo nyimbo nyingine zenye watazamaji wengi ni 'Despacito' ya Luis Fonsi ft. Daddy Yankee una zaidi ya watazamaji bilioni 8 ulitolewa 12 Januari 2017, 'Johny Johny Yes Papa' wa LooLoo Kids (bilioni 7) ulitolewa 15 Mei 2016 huu pia ni wimbo wa watoto unaoonesha hadithi ya Johny na baba yake.

Pia wimbo wa 'Shape of You' wa Ed Sheeran una zaidi ya watazamaji bilioni 6, ulitolewa 30 Januari 2017 na namba tano inashikwa na 'See You Again' wa Wiz Khalifa ft. Charlie Puth una watazamaji zaidi ya bilioni 5.7 ulitolewa 6 Aprili 2015. Wimbo huu ulitolewa kama sehemu ya soundtrack ya filamu ya "Furious 7" na umekuwa na umaarufu mkubwa kutokana na maudhui yake ya kihisia na uzuri wa muziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags