Babu Seya: Chama akija Yanga moto utawaka

Babu Seya: Chama akija Yanga moto utawaka

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking 'Babu Seya' amefurahishwa na tetesi za usajili kwamba huenda kiungo wa Simba, Clatous Chama akajiunga na ‘timu’ ya Yanga, akisema jambo hilo likitokea ‘timu’ hiyo ya wananchi itakuwa haishikiki msimu ujao.

Babu Seya, mzaliwa wa DR Congo, ambaye ameishi Tanzania kwa miaka mingi, anasema yeye ni shabiki wa Yanga tangu mwaka 1972, enzi ambazo alikuwa akimkubali sana za marehemu Gibson Sembuli, gwiji wa Yanga aliyesifika kwa kupiga mashuti makali.

"Mimi naipenda sana timu ya Yanga, mimi ni wa Jangwani bana tangu mwaka 1972, na niseme tu nimefurahishwa sana na tetesi za usajili wa kiungo wa Simba, Clatous Chama kama atajiunga na Yanga timu yetu itakuwa haishikiki," amesema Babu Seya.

Aidha, Babu Seya amesema, anawapenda wachezaji wote wa timu ya Yanga na "Siwezi kubagua nani au nani, maana leo hii nikisema nampenda Aziz KI akiondoka je? Hivyo napenda timu nzima na ndio maana nimedumu kwa muda mrefu kuishabikia timu hii."
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags