Baba wa Neymar akamatwa

Baba wa Neymar akamatwa

Baba mzazi wa mshambuliaji kutoka katika klabu ya PSG Neymar, Neymar de Silva Santos, amekamatwa na mamlaka nchini Brazil, kulingana na ripoti nchini humo.

Inasemekana kuwa mzee huyo alishtakiwa kwa kosa la uhalifu wa mazingira baada ya kudaiwa kufanya kazi iliyopigwa marufuku kwenye jumba la kifahari la Neymar Jr huko Mangaratiba, Brazil.

Kupitia ripoti ya Uol Sport, Santos alikamatwa wakati wa operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya Jiji la Mangaratiba na Polisi wa Kiraia kufuatia malalamiko juu ya uhalifu wa mazingira.

Kukamatwa kwake kulifuatia mabishano na katibu wa mazingira wa Mangaratiba, Shayenne Barreto. Ripoti hiyo imeongeza kuwa Neymar aliachiliwa, lakini wale waliosimamia operesheni hiyo walidai apewe elimu Zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags