Baadhi ya mastaa walivyosherehekea sikukuu ya Christmas

Baadhi ya mastaa walivyosherehekea sikukuu ya Christmas

Haloo weeh!! Haloo tenaa!! Yes kama kawaida yetu bwana ikiwa tunamlizia zile shamrashamra na hekaheka za sikuu ya Christmas bwana tukijiandaa kuupokea mwaka mpya wa 2023 mambo ni moto mambo ni firee.

Yap naweza kusema hivyo bwana lakini kila mmoja ana namna yakusherehekea sikuu kulingana na Imani yake pasi kuingiliwa na mtu yeyote.

Wiki hii kwenye Makala za burudani mtu wangu nimekusogezea mchongo huu hapa uweze kusafisha macho bwana kwa kushuhudia baadhi ya Mastar duniani namna walivyosherehekes sikukuu hiyo na familia zao.

Tukianzia kwenye anga za Michezo bwana huko kimataifa tunakutana na Mchezaji maarufu duniani Mohamed Salah anayechezea timu ya Liverpool akitupia baadhi ya picha kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na familia yake.

 

Aiseee ukiachana na mwamba huyo kwenye football mwengine huyu hapa bwana wanamuita Bruno Fernandes ambaye ni kiungo wa Manchester united naye ametupia picha ya familia yake wakiwa wanasherehekea sikuu hiyo.

 

Tukirudi kibongobongo ama kinyumbani hapa hapa nchini Tanzania bwana kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Clatous Chama  naye aliweka picha ya pamoja na familia yake kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ebwana eeeeh!!! Halikua jambo dogo pia kwa Muigizaji maarufu hapa nchini  Aunty Ezekiel akiwa kwenye sherehe za sikuu hiyo na kupiga picha ya pamoja na familia yake na kutupia kwenye mtandao wa Instagram.

Aloooh hata hivyo mzazi mwenza wa Star wa Muziki wa bongo fleva Diamond Platnumz, bibie Zarina Hassan maarufu Zari thebosslady ameonekana naye kwa kushare picha ya pamoja akiwa na watoto wake bwana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku kuu ya Christmas.

Ebwana eeeh!!!! Wiki hii ni hayo tu kwenye Makala za michezo na burudani name sina mengi Zaidi ya kukutakia Marry Christmas and happy new year tukutane tena 2023 holaaa!!!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags