Baadhi ya Mastaa wakike Bongo wafurahishwa na uvumilivu wa Chioma

Baadhi ya Mastaa wakike Bongo wafurahishwa na uvumilivu wa Chioma

Baada ya mwanamuziki kutoka Nigeria Davido kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Chioma siku ya jana Jumanne Juni 25, mastaa wakike mbalimbali kutoka Bongo wamempongeza Chioma kwa uvumilivu aliouonesha mpaka kufunga pingu za maisha na mkali huyo.

Kupitia kurasa za Instagram za mastaa hao wakike wame-share picha za wanandoa hao na kushusha jumbe tofauti tofauti huku baadhi yao wakiwataka wanawake wa Bongo kuwa na uvumilivu kama wa Chioma.

Moja kwa moja tukianza kwa Mfanyabiashara Niffer kwa upande wake amempongeza Chioma kwa uvumilivu wake.

 “Maisha ni kung’ang’ana tatizo sisi wanawake wa Kitanzania midomooo jaman Zai Kijiwenongwa haoni ndani, Tukio moja tunaenda kasibante Fm kulia na kulaani vikali, na kuita wanaume wote mbwa.

Nimejifunza kitu from my sis Chioma soon nasepa zangu Nigeria na mimi akanifunde kwakweli mwanamke kifua na kufyata mdomo She has been through a looooot yooh acha tu afurahi Ila mimi uvumilivu wake sina, i refuse! You mess with me, you are gone” ameandika

Kwa upande wa dada wa mwanamuziki maarufu Bongo Diamond, Esma Platnumz ameandika “Wakati wa Mungu ni wakati sahihi usikate tamaa, kuwa kama Chioma ni kazi rahisi sana je huyo ulokuwa nae anaweza kuwa kama Davido au zaidi ya Davido”

Ukiachilia mbali ya Esma kuwatia moyo wanawake wasikate tamaa kwa mwigizaji Faymah ‘Fayvanny’ amefurahiswa na Chioma huku akimshukuru kwa kumnyooshea ma-side cheack.

“Chioma amethibitisha kwamba ving’ang’a tuna nguvu kiasi gani haya nyie mnao kuwa na wanaume kwa muda mfupi mfano mzuri mmepata kwa Davido, mwanaume anaweza kuchepuka na wewe ila haimaanishi anakupenda, Chioma asante kwa kuninyooshea ma side chieck wote” ameandika Fayvanny                                  

Davido na Chioma walikutana kwa mara ya kwanza walipokuwa chuo kikuu huku kwa mujibu wa Davido katika moja ya mahojiano yake mwaka jana alidai kuwa alianza mahusiano ya kimapenzi na Chioma mwaka 2013.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags