Baada ya siku 365 Profesa Jay arudi studio

Baada ya siku 365 Profesa Jay arudi studio

Msaani wa miondoko ya Hip-Hop, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ameonekana akiwa studio akirekodi nyimbo ikiwa ni baada ya mwaka mmoja tangu atoe nyimbo ya “Hands Up” aliyomshirikisha G-Nako.

Jay ameonekana akiwa studio kwa Binladen ambapo aliandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii uliosomeka; “Asante Mungu, back to the business again, Studio session with my young brother Binladen,”

Ikumbukwe tu januari 2022 tangu alipoanza kupigania maisha yake akiwa kitandani lakini alijitokeza tena hadharani mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu baada ya kupona.

Kwa kuchapisha jumbe kwenye mitandao yake ya kijamii akimshukuru Mungu pamoja na wale waliokuwa pamoja nae wakiwemo madaktari , ndugu, marafiki, wasanii wenzake na viongozi kwa maombi na misaada yao iliofanikisha leo hii amesimama tena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags