Baada ya Danny kufungwa miaka 30 kwa ubakaji, Ndoa yake na Bijou yavunjika

Baada ya Danny kufungwa miaka 30 kwa ubakaji, Ndoa yake na Bijou yavunjika

Wasanii kutokea nchini Marekani Bijou Phillips na Danny Masterson wapeana talaka baada ya ndoa yao kuingia doa.

Inadaiwa Bijou amefanya uamuzi wa kukatisha ndoa yake baada ya mumewe Danny kupata kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji.

Kulingana na hati za kisheria, zilizopatikana, Bijou aliwasilisha kesi ya madai ya talaka hiyo siku ya Jumatatu katika mahakama ya California nchini humo.

Aidha wanandoa hao watahusiana kwenye malezi ya mtoto wao tu, mwenye umri wa miaka 9, huku Bijou akidai kuwa yuko tayari kumuacha mtoto amtembelee baba yake lakini kwa ulinzi wa kusheria.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags