Azika mtoto akiwa hai kisa kupata utajiri

Azika mtoto akiwa hai kisa kupata utajiri

Binti mmoja mkazi wa kijiji cha Mahaha, wilayani Magu, mkoani Mwanza, Zawadi Msagaja (20) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumzika mtoto akiwa hai ili apate mali (utajiri).

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema watuhumiwa wanadaiwa kutenda unyama huo Novemba 13 mwaka huu mchana katika mtaa wa Kisundi, kata ya Bugogwa, wilayani Ilemela, mkoani humo.

Aidha wengine wanaoshikiliwa katika tukio hilo ni dada yake Zawadi, Elizabeth Kaswa na mumewe, Mussa Mazuri ambaye ni mganga wa kienyeji aliyetoa maagizo ya kutekeleza kitendo hicho huku akimtishia Zawadi kuwa asipofanya hivyo yeye ndiyo atatolewa kafara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags