Ayra Starr, Tems vinara Spotify

Ayra Starr, Tems vinara Spotify

Wanamuziki maarufu wa Nigeria, Ayra Starr na Tems wametangazwa kuwa mwaka huu nyimbo zao ndio zinasikilizwa zaidi kutokea nchini humo kupita Jukwaa la Spotify.

Inaelezwa kuwa jukwaa la kimataifa la kutiririsha muziki limeonesha wasanii hao nyimbo zao zipo kwenye orodha ya 30 bora huko Nigeria zinazosikilizwa zaidi mwaka 2024.

Ayra Starr ameshika nafasi ya pili kupitia wimbo wake wa ‘Comma’ huku Tems akikamata nafasi ya tatu katika ngoma ya ‘Love Me Jeje’.

Wimbo wa Luciano na Omah Lay unaokwenda kwa jina la 'Another Vibe' umeshika nafasi ya tatu huku 'Just Like Me’ ulioimbwa na 21 Savage, Burna Boy na Metro Boomin ukishika nafasi ya tano kwa kutiririshwa.

Phiona Okumu ambaye ni mkuu wa Spotify Kusini mwa Jangwa la Sahara, ameeleza kuwa orodha hiyo ilitambua nyimbo za Wanigeria zilizosikilizwa zaidi kutoka nje ya nchi kati ya Januari 1 na Juni 30, 2024.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags