Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Ayra Starr amepewa shavu na mwanamuziki Chris Brown kuwepo kwenye ziara yake iliyopewa jina la ‘11:11’ ambayo imebeba jina la album ya Brown.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Breezy ame-share taarifa hiyo ambapo mwadada Ayra Starr atakuwa kwenye ziara ya Breezy katika miji 26 ikiwemo Canada, Marekani, Washington DC, Toronto na mingineyo.
Ziara hiyo inatarajiwa kuanzia mjini Detroit Juni 5 na kumalizika Los Angeles, Agosti 6 mwaka huu 2024, Chris Brown anamualika Ayra Starr kama mgeni maalum ‘Special Guest’ katika tour hiyo, huku samnii mwingine akiwa ni Muh Knee Long.

Leave a Reply