Aweka rekodi ya kukaa kwenye barafu kwa saa 3

Aweka rekodi ya kukaa kwenye barafu kwa saa 3

Mwanamke mmoja kutoka nchini Poland aitwaye Katarzyna Jakubowska (48) ameweka rekodi ya dunia ya ‘Guinness World Records’ kwa kukaa kwenye sanduku la barafu kwa muda mrefu.

Katarzyna ameingia katika kitabu cha Guinness kwa kuwa mwanamke wa kwanza kukaa ndani ya barafu kwa saa 3 dakika 6 na sekunde 45.

Hapo awali Krzysztof Gajewski ndiye aliyekuwa akishikiria rekodi hii kwa upande wa wanaume, ambapo alikaa ndani ya sanduku la barafu kwa saa 3 na dakika 11 na sekunde 27, akiipiku rekodi ya Wim "The Iceman" Hof aliyekaa kwa saa 1tu.

Kwa mujibu wa mwanamama huyo alieleza kuwa kabla ya kutaka kuweka rekodi hiyo alifanyiwa vipimo mbalimbali vya matibabu kuhakikisha ahatarishi afya yake, hata hivyo alisema kuwa alifanya mazoezi mara tatu ya kujaribu kukaa kwenye barafu kwa muda mrefu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags