Avunja rekodi ya kucheza Chess kwa saa 60

Avunja rekodi ya kucheza Chess kwa saa 60

Bingwa wa mchezo wa chess kutoka nchini Nigeria, Tunde Onakoya ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuvunja rekodi ya kucheza chess kwa saa 60 mfululizo mchezo uliyochezwa Times Square jijini New York.

Wakati akisubiri uthibitisho kutoka kwa shirika la Rekodi ya Dunia ya Guinness, kazi ya Onakoya tayari imemfanya kuwa shujaa nchini Nigeria, ambapo ameweka wazi kuwa lengo la kutaka kuvunja rekodi hiyo ni kukusanya dola 1 milioni kwa ajili ya kuwapatia elimu watoto wote wenye uhitaji Afrika.

Hapo awali rekodi hiyo ilishikiliwa na Hallvard Haug Flatebø na Sjur Ferkingstad kutoka Norway ambapo walitumia saa 56 dakika 9 na sekunde 37 mchezo uliyochezwa mwaka 2018.

Aidha nyota huyo aliungwa mkono na watu mbalimbali akiwemo mkali wa Afrobeat Davido ambaye alifika eneo la tukio na kumsapoti Onakoya pamoja na Rais wa Nigeria Bola Tinubu kumpongeza kwa hatua aliyoichukua.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags