Avunja rekodi ya dunia kwa kupika masaa mengi

Avunja rekodi ya dunia kwa kupika masaa mengi

Mpishi kutoka Nigeria, Hilda Effiong Bassey, maarufu kama Hilda Baci, amevunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa mbio ndefu zaidi za upishi za mtu binafsi.

Mpishi huyo, leo Jumatatu asubuhi, alivunja rekodi ya saa 87 na dakika 45 iliyowekwa na mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya Guinness, Lata Tondon.

Mwanadada huyo alipaswa kupika siku 4 mfululizo (saa 96) bila kupumzika. ambapo mpaka sasa amebakisa masaa 6 tuu kumaliza shindano hilo.

Baadhi ya vitu ambavyo alitakiwa kuzingatia kwenye shindano hilo ni kama vile. lazima asimame akiwa anapika, hatakiwi kukaa, hatakiwi kutumia kahawa au kinywaji chochote cha kumuongezea nguvu kama (energy drinks), ni ruksa kunywa, kula na kutumia glucose, siku 4 bila kulala kabisa, dakika 5 tu za kupumzika kila lisaa.

Na kila atakachopika anapaswa agawe bure chakula kwa wateja na sio kuwauzia, kupika chakula cha aina yoyote ile anachopenda wala hakuna sheria ya kumpangia cha kupika, kila chakula atakachopika na kila sahani itakayotolewa kwa mteja inawekwa kwenye rekodi kama (kumbukumbu).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags