Auwawa kwenye  maandamano ya kupinga  serikali mpya Peru

Auwawa kwenye maandamano ya kupinga serikali mpya Peru

Taarifa kutoka nchini Peru ambapo Maandamano dhidi ya serikali mpya nchini humo  yameendelea kuutikisa mji mkuu, Lima, huku mvulana mmoja akiuawa.

Aidha Waandamanaji waliingia tena mitaani mwishoni mwa wiki wakidai uchaguzi mpya na kuachiwa mara moja kwa rais aliyeondolewa madarakani, Pedro Castillo.

Tangu bunge kumuondowa madarakani Rais Castillo siku ya Jumatano alipojaribu kulivunja bunge hilo, maandamano yamesambaa kote nchini humo. Dina Boluarte, aliyekuwa makamu wa rais wa Castillo, aliapishwa haraka kuchukuwa nafasi ya urais, lakini waandamanaji wanamtaka ajiuzulu haraka.

 Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Maandamano ya jana Jumapili yaligeuka vurugu, baada ya waandamanaji kukabiliana na polisi katika mji wa kusini wa Andahuaylas. Raia 16 na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa kwenye mji huo siku ya Jumamosi.

Serikali mpya iliyotangazwa na Boularte ilitazamiwa kukutana na bunge kwenye mkutano wa dharura kujadiliana hatua za kukabiliana na wimbi kubwa la maandamano ya umma.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags