Atumia zaidi ya Million 49 ili afanani na mbwa

Atumia zaidi ya Million 49 ili afanani na mbwa

Mwanaume mmoja kutoka nchini Japan alioyefahamika kwa jina la Toco ametumia zaidi dola 20,000 ambazo ni zaidi ya sh 49 milioni za kitanzania ili kuwa na muonekano wa mbwa.

Alifanya hivyo ili kutimiza ndoto yake ya maisha kujibadilisha na kuwa na muonekano wa mnyama huyo ndipo akaamua kutumia pesa hizo kununua vazi lenye kumpa muonekano wa mbwa.

Mwanaume huyo aliagiza vazi hilo kwenye kampuni ya Kijapani iitwayo Zeppet, ambayo imejikita na masuala ya sanamu na mifano ya filamu, matangazo na vifaa vya burudani pamoja na mavazi ya TV na mascots, inasemekana kuwa vazi hilo lilichukua siku 40 kutengenezwa hadi kukamilika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags