Asilimia 7 ya watanzania wanaugua figo

Asilimia 7 ya watanzania wanaugua figo

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema asilimia 7 ya Watanzania wanaishi na ugonjwa wa figo huku akitoa rai kwa Wananchi kupima ugonjwa huo mara kwa mara ili kuepuka madhara yake makubwa ikiwemo gharama kubwa ya matibabu yake.

Waziri huyo amesema hayo leo May 19, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge Asia Abdukarimu Halamga katika Mkutano wa 11 kikao cha 29, Bungeni Jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa unahusishwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa kisukari na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Mollel amesema katika kujali afya za Watanzania wakiwemo wenye ugonjwa wa figo, Serikali ya Rais Samia imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 290.9 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali za Mikoa ambapo katika vifaa hivyo vipo vifaa vya matibabu ya kusafisha damu (dialysis) kwa Wagonjwa wa figo.

Aliendelea kwa kusema kuwa, Serikali ipo katika mpango wa kuona namna ya kupunguza gharama ya matibabu ya figo kupitia huduma ya kusafisha damu ili Wananchi wenye uhitaji waweze kunufaika na huduma hizo, huku akiweka wazi kuendelea kuwatazama wasio na uwezo kabisa kupitia njia ya misamaha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post