Mfanyabiashara maarufu nchini Aristote amefunguka namna biashara yake ya saluni inavyomnufaisha huku ikimpatia furasa nyingine ambayo imekuwa ikimlipa zaidi kwa sasa.
Akizungumza na Mwananchi Aristote ameeleza kuwa biashara ya saluni imekuwa kama muhimili kwa upande wake ambapo kwa muda alikuwa akikusanya mapato ya saluni yake na kuwekeza kwenye sekta ya nyumba inayomlipa na kufanya aendelee kutamba mjini.
“Uwekezaji wa nyumba umeongeza kipato changu kwa kiasi kikubwa. Ni biashara yenye faida kubwa kama ukiwa na dhamira, lakini pia Mitandao ya kijamii inanisaidia sana. Kwa kushiriki kazi zangu, nimefanikiwa kutoka sifuri hadi kuwa maarufu,” amesema Aristote
Mbali na hayo pia amefunguka kuhusiana na baadhi ya wadau katika mitandao ya kijamii wanaumsema vibaya kuhusiana na mwanaume kufanya kazi katika saluni za wanawake ambapo anaeleza kuwa yeye haangalii masimango ya watu bali kwake anaichukulia kama Sanaa.
“Watu wanadhani ni jambo la kushangaza, lakini kwangu, ususi ni sanaa ya ubunifu, na ubunifu haupaswi kuwekwa mipaka kwa jinsia, Duniani kote, baadhi ya ikoni maarufu za mitindo ni wanaume. Ni wakati wa jamii kuacha mawazo haya ya kizamani.” Alisisitiza Aristote
Aristote, Mtanzania mwenye asili ya Congo alianza kujifunza kutengeneza nywele kwenye saluni za wanawake bila kuwa na uzoefu wowote, alifanya kazi kwa muda ndipo akafungua saluni yake mwenyewe na baada ya muda aliona biashara yenye faida ni kuuza nywele halisi ambapo aliwekeza dola 3,000 na kusafiri kwenda kufuata mzigo China.
Mfanyabiashara huyo ambaye anasafiri China na Vietnam, kufuata nywele asili (Human Wigs) ameshawahi kutengeneza vichwa vya mastaa kutoka ndani nan je ya Nchi kama Elizabeth Michael (Lulu), Zari Hassan, Tanasha Donna, Wema Sepetu, Irene Uwoya, na Shilole,na wengineo.
Leave a Reply