Apple yatuhumiwa kutumia madini ya wizi

Apple yatuhumiwa kutumia madini ya wizi

Serikali ya Congo imeishutumu Kampuni ya Apple kwa kutumia Madini yaliyochimbwa kinyume na sheria Mashariki mwa nchi hiyo kutengeneza bidhaa zake.

Kupitia mawakili wa nchi hiyo wameionya kampuni hiyo kuwa inaweza kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa itaendelea kuyatumia madini hayo.

Pia mawakili hao wanaishutumu Apple kwa kununua madini yaliyotoroshwa kutoka DRC na kusafirishwa hadi nchi ya Rwanda ambayo imekuwa ikishutumiwa kwa wizi wa madini.

Hata hivyo kwa upande wa kampuni hiyo imekanusha shutuma hizo kwa kudai kuwa hakuna ushahidi wowote kuhusu madini hayo kuibiwa DRC.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags