Apigwa risasi na kuuwawa akidhaniwa ni sungura

Apigwa risasi na kuuwawa akidhaniwa ni sungura

Mwanamume mmoja raia wa China amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mwindaji ambaye alidhania kuwa ni sungura.

Adlyne Wangusi Moujin alianguka kwenye shimo baada ya kupigwa risasi kichwani na bunduki ya anga, Mwindaji huyo alifyatua risasi baada ya kuona msogeo kwenye nyasi kando ya bwawa, ambapo Moujin aliripotiwa kuwa akivua samaki.

Wanaume wanne wamekamatwa kuhusiana na kifo hicho kilichotokea mnamo Ijumaa, Aprili 14, wakati wanne hao walipoenda kuwinda katika Mji wa Shaxi, mkoa wa Jiangxi.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi katika wilaya ya Xinzhou, walisema mmoja wa watu hao alifyatua risasi baada ya kuona msogeo kwenye nyasi kando ya mtaro, ambapo aliripotiwa kuwa akivua samaki.

Polisi walifika kwenye eneo la tukio na kuwakamata wanaume hao wanne, ambao baadhi yao wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 30. Huku uchunguzi wa maiti ulibaini kuwa Moujin alifariki kutokana na kuzama kwenye maji.

Chanzo Tuko






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags