Apigwa na watoto wake baada ya kuolewa na mwanaume mwingine

Apigwa na watoto wake baada ya kuolewa na mwanaume mwingine

Mama mmoja kutoka nchini Kenya amepigwa na watoto wake waliopandwa na hasira walipoona amemuacha baba yao na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo, wamepigwa yeye na mume wake ambao kwa sasa wanauguza majeraha wote.

Inadaiwa kuwa wanandoa hao kutoka kaunti ya Samburu walivamiwa na watoto waliokuwa na silaha na kumuacha baba yao huyo wa kambo akiwa kipofu kutokana na kumtoboa macho.

“Niliaibika, walivamia nyumba yetu na kuanza kunipiga kisha wakamwendea mume wangu baada ya kumkuta ndani ya nyumba hiyo, wakamvamia machoni mwake” amesema mama huyo aliyetambulika kwa jina la Sylevena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags