Amteka mtoto wa ex wake, akitaka hela

Amteka mtoto wa ex wake, akitaka hela

Mwanaume mmoja kutoka nchini Marekani, Richard White, mwenye umri wa miaka 36 anashikiliwa na polisi kwa madai ya kumteka nyara mtoto wa ex wake mwenye umri wa miaka mitano, mleze wa mtoto huyo na mpenzi wa mlezi wa mtoto huyo baada ya kuwa na ugomvi wa muda mrefu na aliyekuwa mpenzi wake.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alikuwa akitaka pesa kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake, hivyo kutokana na topatiwa pesa hizo akaamua kuchukua uamuzi wa kuwateka watu hao watatu kwa lengo la kumkomoa ex wake.

Kwa upande wa mwanamke huyo ambaye anafanya kazi kwenye moja ya ‘klabu’ nchini humo, amedai kuwa alipokea simu na jumbe za vitisho kutoka kwa ex wake huyo, na aliporudi kutoka kazini aligundua kuwa mtoto wake na walezi wa mtoto huyo ambao walikuwa wapenzi hawapo nyumbani na baada ya kufuatilia kwenye CCTV camera aligundua kuwa mwanaume huyo aliwateka watu hao wote watatu.

Idara ya Polisi ya Bloomington imethibitisha kumshikilia mwanaume huyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mama wa mtoto huyo akieleza kuwa White alikuwa amefungua mlango wake wa mbele wa nyumba na kuwateka watu watatu waliokuwa nyumbani hapo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags