Ally Mayay ateuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo

Ally Mayay ateuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo

Alooooh! Mambo yanazidi kuwa mazuri kwa upande michezo, naona sasa hivi wameamua kumleta yule nguli katika michezo kitambo sana. Basi bwana, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imemtangaza mkongwe wa Taifa Stars na mchambuzi mahiri wa soka, Ally Mayay Tembele kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya michezo nchini, akichukua nafasi ya Yusuph Omary Singo aliyepangiwa majukumu mengine.

Aidha Taarifa ya Wizara imesem,a "Uteuzi huu unaanza leo Septemba 20 2022, Wizara inamtambulisha Ally Mayay Tembele kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini wakati taratibu nyingine zikiendelea.”

“Mayay ambaye ni Afisa Mwandamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini amehamishiwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuruhusiwa kukaimu haya kwa mujibu wa kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Wadau wa michezo wanaombwa kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake," imeeleza taarifa hiyo.

Angusha komenti yako hapo chini, je hiki cheo Mr Tembele kinamfaa na atakitendea kazi kama ipasavyo? Usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa moto moto.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post