Aliyetumia fedha za kampuni kula bata ahukumiwa miaka mitano jela

Aliyetumia fedha za kampuni kula bata ahukumiwa miaka mitano jela

Aliyekuwa Meneja wa programu za #Facebook, Barbara Furlow-Smiles, ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya ulaghai baada ya kuiba zaidi ya dola 5 milioni kutoka kwa kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Hukumu hiyo ilitangazwa rasmi na Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani siku ya Jumatatu wiki hii.

Shughuli hizo za ulaghai za Barbara Furlow-Smiles zilianza wakati wa utumishi wake kama mtendaji mkuu wa DEI Facebook, ambapo alianza kazi katika kampuni hiyo mwaka 2017 hadi 2021.

Aidha Desemba mwaka jana mwanadada huyo alikiri kosa kwa kueleza kuwa alitumia fedha hizo kuendesha maisha yake ya kifahari aliyokuwa akiishi California.

Waendesha mashitaka walieleza kuwa #Furlow-Smiles alitekeleza utapeli huo kwa kufanya malipo kwa niaba ya #Facebook kwenda kwa marafiki, jamaa na washirika wengine kwa bidhaa na huduma ambazo hazikutolewa kwenye kampuni hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags