Aliyeshikilia rekodi ya kuwa na kucha ndefu afariki

Aliyeshikilia rekodi ya kuwa na kucha ndefu afariki

Mwanamama kutoka nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la Lee Redmond ambaye alikuwa akishikilia rekodi ya Guinness World Records kwa kuwa na kucha ndefu zaidi afariki dunia.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Guinness World Records ume-share taarifa ya kifo cha mwanamama huyo kwa kueleza kuwa imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Lee ambaye ameshikilia rekodi kwa miaka mingi ya kuwa na kucha ndefu zaidi Duniani.

Lee Redmond alikuwa na kucha zenye urefu wa 7 m 51.3 cm (24 ft 7.8 in) mwaka 2003 na rekodi yake ikavunjwa na Diana Armstrong mwaka 2022.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags