Aliyepigwa na Tyson Apata Mwanasheria

Aliyepigwa na Tyson Apata Mwanasheria

Waswahili wanasema ukimwa mboga wenzako wanamwaga ugali, au msemo mwingine unasema hivi kama mbwai mbwai tu  hiki ndicho kimetokea baada ya bondia maarufu duniani Mike Tyson kumpiga vitasa abiria kwenye ndege wiki hii.

Taarifa kutoka New York Post inaripoti  kuwa Abiri wa ndege ya JetBlue aliyepigwa ngumi na Mike Tyson amepata wakili wa kumuwakilisha katika kesi yake inayotajwa kuwa ya madai ya fidia kutoka kwa bondia huyo.

Sasa bwana Wakili wa Abiria huyo amezungumza haya  "Mteja wangu ni shabiki mkubwa wa Mike Tyson".

Nikukumbushe tu kuwa Wiki hii video ilisamba ya Tyson akigombana na abiria kwenye ndege ambapo baadae mashahidi walisema 'Alikuwa shabiki aliyepitiliza kuwa na furaha [Overly Excited Fan ] alikuwa na shauku kubwa na kumuona Tyson akajisahau na kumsumbua zaidi".







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags