Aliyepanga njama ya kumuua AKA ajulika

Aliyepanga njama ya kumuua AKA ajulika

Mahakama nchini Afrika Kusini imemtaja mfanyabiashara, Sydney Munda Gcaba kuwa ndiye mtu aliyewalipa watuhumiwa sita wa mauaji ya aliyekuwa ‘rapa’ Kiernan Forbes, maarufu kama #AKA ambapo anadaiwa kuwalipa tsh 108 milioni kwa ajili ya kutekeleza mauaji hayo.

Kwa mujibu wa #News24 imeeleza kuwa Februari 11, 2023 saa sita mchana mmoja wa wauaji aliyefahamika kwa jina la #Gwabeni alipokea pesa hizo kwenye akaunti yake na inadaiwa kuwa alizitoa na kugawana na washirika wenzie.

Washukiwa waliyokamatwa wiki kadhaa zilizopita walikuwa ni Siyanda Myeza (21), Lindokuhle Ndimande (29), Lindani Ndimande (35), ambao ni mtu na kaka yake, Lindokuhle Thabani (30) na Mziwethemba Myeza (36).

Ikumbukwe kuwa AKA alifariki yeye na rafiki yake wa karibu mpishi maarufu na mjasiriamali #Tebello February 10, mwaka jana mjini Durban nchini humo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags