Aliyefanya upasuaji wa matiti, Midomo, na kubadili rangi awe muafrika

Aliyefanya upasuaji wa matiti, Midomo, na kubadili rangi awe muafrika

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kumekuwa na matukio mengi ya kisayansi yafanyikayo ikiwemo baadhi ya watu mkubadiisha mionekano yao, kama vile kuongeza maumbo, kujibadili rangi na mengine mengi.

Katika maeneo mengi imezoeleka baadhi ya watu wenye ngozi nyeusi hutumia vipodozi kuwa na ngozi nyeupe, hii imekuwa tofauti kwa mwanamitindo Martina Big raia wa Ujerumani ambaye alifanya upasuaji mara kadhaa kubadili muonekano wake kuwa wa kiafrika na ngozi kuwa nyeusi kabisa.

Martina Big, alikuwa na shahuku ya kuwa na muonekano wa kiafrika na kuamua kufanya upasuaji wa kuongeza matiti yake, kuongeza ‘lips’ pamoja na kudunga sindano za kubadilisha ‘homoni’ ili rangi ya ngozi yake kutoka kuwa nyeupe hadi nyeusi.

Mwaka 2012 akiwa na umri a miaka 23 alianza kufanya upasuaji wa kuongeza matiti, huku mwaka 2017 aliamua kubadili muonekano wa ngozi yake na kuwa nyeusi, hakuishia hapo kila baada ya miezi kadhaa Big amekuwa ni mtu wa kuboresha mwili wake.

Baada ya kufanya mabadiliko kadhaa mwaka 2018 alisafiri kuelekea nchini Kenya kwa ajili ya kuanza maisha katika jamii ya maasai na Samburu ambako huko walimbaatiza jina na kumuita Malkia Kubwa.

Kati ya vitu ambavyo amekuwa akiwashangaza wengi ni kudai  ‘daktari’ wake alimueleza kuwa anaweza akaja kupata watoto weusi japo yeye na mume wake asili yao ni ngozi nyeupe, pia katika hatua zote za kujibadilisaha alizopita amekuwa akishirikiana na mume wake bega kwa bega.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags