Aliomba talaka kwa sababu mumewe hakuwa msaliti

Aliomba talaka kwa sababu mumewe hakuwa msaliti

Mwanamuziki kutoka nchini Brazil Caroline Lyra ambaye pia alikuwa mke wa zamani wa mchezaji Ricardo Kaka, amedai kuwa aliomba talaka kwa mumewe kwa sababu hakuwa akimsaliti wakati walipokuwa kwenye ndoa.

Caroline amenukuliwa na ‘All Things Brazil media’ akieleza kuwa Kaka hakuwai kumsaliti hata mara moja alikuwa mtu mwema kwake na alifanya kila kitu kwa ajili ya familia licha ya yote hakuwahi kufurahia ndoa yao kutokana na mumewe kuwa mkamilifu sana kwake.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005 na kutangaza kuachana kupitia mitandao ya kijamii mwaka 2015, ambapo walibahatika kupata watoto wawili.

Ricardo Kaka alistaafu kucheza soka mwaka 2017, akichezea ‘timu’ mbalimbali zikiemo ‘Real Madrid’, ‘Orlando City’, ‘AC Milan’ akicheza zaidi kama kiungo mshambuliaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags