Alimchumbia Kim Kardashian na akaachwa

Alimchumbia Kim Kardashian na akaachwa

Siku hazigandi na mapenzi nayo huwa yana mwisho.

Comedian maarufu Marekani, Pete Davidson ameripotiwa kuwa alimchumbia mfanyabiashara Kim Kardashian kabla ya kuachana kwao.

Wawili hao waliokuwa kwenye mahusiano kwa takriban miaka 9, walitaja sababu za kuwa na muda mchache wa kuonana, pamoja na kuwa na ratiba nyingi kama sababu ya kushindwa kuendelea na mahusiano yao.

"Vitu Vilikuwa Vinaenda Haraka Sana. Kim Alitaka Mambo Yaende Taratibu Lakini Pete Alimchumbia" - Chanzo Kiliiambia RADAR. "Yani Alichanganyikiwa Na Kila Mmoja Alimuonya Kuwa Ataachwa Lakini Hakusikia Kabisa."

Pete aliwahi kumchumbia msanii Ariana Grande kipindi cha nyuma baada ya kudate kwa wiki kadhaa tu.

Hata hivyo, uhusiano kati ya Pete na Kim ulikuwa haushiwi vituko kwani aliyekuwa mume wa Kim, Kanye West alikuwa na vita kali na wawili hao na kuwapa wakati mgumu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags