Al Ahly sio kinyonge, Watua na mchezaji mpya

Al Ahly sio kinyonge, Watua na mchezaji mpya

‘Klabu’ ya #Al Ahly, ambao ni mabingwa nchini Misri, inaelezwa kuwa wamefanikisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Borussia Dortmund, Anthony Modeste, aliyejiunga kwa uhamisho huru.

Mchezaji huyo inadaiwa ametia ‘saini’ ya mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi kama akipenda.

Aidha mshambuliaji huyo amekuwa mchezaji huru tangu aachane na #Dortmund mwezi Juni mwaka huu, huku mkataba wake na ‘timu’ ya  Al Ahly, utamfanya raia huyo wa Ufaransa apokee takribani dola milioni 1.5 kwa msimu, huku kukiwa na ‘bonasi’ zitokanazo na kiwango atakacho kionyesha uwanjani.

Ikumbukwe mwezi huu ‘klabu’ ya Al Ahly wamepangwa na ‘klabu’ ya Simba Sports Club ya Tanzania kwenye michuano ya African Football League, na huenda mshambuliaji huyo mpya akawa sehemu ya kikosi hicho kitachocheza na mnyama siku Jumamosi tarehe 16 mwezi huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags