Akoni mbioni kupokonywa ardhi ya mji wake

Akoni mbioni kupokonywa ardhi ya mji wake

Imeripotiwa kuwa ardhi ya mwanamuziki kutoka Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon muda wowote kuanzia sasa inaweza kuchukuliwa na Serikali ya Senegal, endapo hatokamilisha mapema ujenzi wa mji wake.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali vimeripoti kuwa Serikali ya Senegal imemtumia barua ya kutaka msanii huyo aendelee na ujenzi wa mji wake huo unaodai kugharimu Sh 16 Trillioni.

Utakumbuka kuwa mwaka 2018 Akon alipewa ardhi hiyo na aliyekuwa rahisi wa nchi hiyo Macky Sall, ambapo Akon alitangaza kujenga mji wake utakaoitwa ‘Akon City’ ambao mji huo utatumia sarafu yake ya ‘Akoin’ huku akitangaza kuweka majengo makubwa ya biashara, viwanda, shule za muziki na burudani pamoja na mahitaji yote muhimu.

Aidha kufuatia na taarifa hiyo mmoja wa ndugu wa karibu wa Akon alifunguka na kudai kuwa msanii huyo bado hana taarifa kuhusu barua hiyo.

Hata hivyo kupitia barua hiyo Serikali ya Senegal imemtaka Akon kutimiza ahadi yake ya kujenga mji huo kama walivyo kubaliano kwani baadhi ya wakazi wamekuwa wakisubiri mji huo kukamilika kwa muda mrefu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags