Akon: Diddy anahitaji maombi

Akon: Diddy anahitaji maombi

‘Rapa’ na mwigizaji kutoka nchini Marekani Akon amefunguka machache kuhusiana na sakata linalo mkabili mwanamuziki Diddy la kuhusishwa na biashara ya ngono huku akiwataka mashabiki na wadau mbalimbali kumuombea Combs.

Akizungumza na Tmz, Akon ameeleza kuwa yeye siyo mtu wa bata sana wala kutoka kwa hivyo hajui kuhusiana na yanayoendelea kwenye Party za Diddy lakini anatumai ukweli wote utadhihirishwa na kila mtu atapata stahiki yake.

Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa kwa sasa Diddy anahitaji maombi hivyo ni vyema watu kumuombea na kumuachia Mungu suala hilo kuliko kuendelea kumshambulia kupitia mitandao ya kijamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags