Akili bandia yatumia kudanganya uwepo wa Rihanna Met Gala

Akili bandia yatumia kudanganya uwepo wa Rihanna Met Gala

Baada ya kuripotiwa kuwa mwanamuziki Rihanna hakuweza kuhudhuria katika tamasha la mitindo la ‘Met Gala’ lililofanyika nchini Marekani, baadhi ya watu wametengeneza picha ‘feki’ za msanii huyo kwa kutumia AI (Akili Bandai) wakidai kuwa Riri alikuwepo katika maonesho hayo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini Marekani vimethibitisha kuwa mwanamuziki huyo hakuwepo katika maonesho hayo huku wakiwataka mashabiki wa mataifa mengine kupuuzia uvumi huo.

Hata hivyo kupitia ukurasa wa Instagram wa Katy Perry ame-share picha hiyo iliyotengenezwa na AI na kukanusha kuwa mwanamuziki huyo hakuwepo kwenye ‘Met Gala’ kutokana na kuwa na kazi nyingi.

Picha nyingine za mastaa ambao zimetengenezwa kwa kutumia AI (Akili Bandia) na Katy Perry, na Lady Gaga.

Ikumbukwe kuwa tovuti ya People ilidai kuwa ilimtafuta mmoja wa watu wa karibu wa Riri ambapo alidai kuwa mwanamuziki huyo aliamua kughairisha kuhudhuria tamasha hilo kutokana na kuumwa na mafua.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags