Ajiziba uso ili aache kuvuta sigara

Ajiziba uso ili aache kuvuta sigara

Kuacha sigara ni mchakato ambao baadhi ya watumiaji wamekuwa wakigonga mwamba kila uchwao, lakini kwa Ibrahim Yücel kutoka Uturuki ilikuwa rahisi baada ya kutengeneza kofia ya chuma iliyokuwa ikifungwa na kufuri.

Baada ya baba yake mzazi kufariki mwaka 2013 na kansa ya mapafu iliyosababishwa na uvutaji wa sigara alitafuta mbinu ya kuachana na uraibu huo kwa kuvaa kofia iliyotengenezwa na chuma ambayo ilikuwa ikifungwa na kufuri huku funguo akimkabidhi mkewe na mtoto wake.

Yücel, ambaye alikuwa akivuta pakiti mbili za sigara kwa siku kwa miaka 26, alifanya uamuzi huo ili kujizuia kuvuta sigara wakati wa mchana akiwa kazini.

Hata hivyo kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vilieleza kuwa mwanaume huyo alifanikiwa kuacha uvutaji wa sigara ndani ya miezi michache huku baadhi ya majirani zake wakimpongeza kwa juhudi hizo kufanikiwa baada ya kujaribu kwa mara kadhaa kuachana na uraibu huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post