Ajichoma sindano ya damu ya boyfriend mwenye ukimwi kukomoa wazazi

Ajichoma sindano ya damu ya boyfriend mwenye ukimwi kukomoa wazazi

Wahenga husema mapenzi ni upofu na hili limethibitishwa na binti wa miaka 15 huko nchini India ambaye alichukua maamuzi wa kujichoma damu ya mpenzi wake mwenye virusi vya ukimwi ili kuonesha wazazi wake kuwa yuko kwenye penzi zito na hatoachana nae.

Binti huyo anayetokea katika kijiji cha Suwal Kuchchi, Assam alikutana na boyfriend wake, mkazi wa Hajo kupitia mtandao wa Facebook. Mapenzi yao yalikua baada ya kuwa na mazungumzo kadhaa.

Kutokana na chaneli moja nchini humo, wawili hao wamekuwa pamoja kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya binti huyu kuchukua maamuzi hayo magumu. Inasemekana kuwa binti huyo alishawahi kujaribu kutoroka nyumbani hapo nyuma, hata hivyo wazazi wake walifanikiwa kumrudisha.

Baada ya familia yake kutilia mkazo sana katika yeye kuachana na mwanaume huyo, Binti akaamua kumtoa mpenzi wake damu na kujichoma mwenyewe ili kuthibitisha penzi lake hilo. Baada ya familia kugundua kuhusiana na hilo, walimfungulia mashtaka mwanaume huyo ambaye baadae alitiwa mbaroni.

 

ANGALIZO: Mwananchi Scoop haisapoti vitendo vyovyote vinavyoongeza kusambaza ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi unaua, kuwa makini, jilinde.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags