Ahmed Ally: Wydad ni mnyama aliyesinzia

Ahmed Ally: Wydad ni mnyama aliyesinzia

Afisa Habari na Mawasiliano wa ‘klabu’ ya #SimbaSC, #AhmedAlly amedai kuwa ‘klabu’ ya #Wydad ni mnyama mkali aliyesinzia hivyo wanatakiwa kujiandaa kukabiliana nao katika ‘mechi’ ya ‘ligi’ ya mabingwa #Afrika inayotarajiwa kuchezwa Desemba 9

Ahmed ameyasema hayo kupitia ukurasa wa Instagram ameandika ujumbe kuwa kikosi chao kinarejea kambini leo kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya ‘klabu’ ya #WaydadCasablanca.

Hata hivyo ameeleza kuwa mpinzani wao japo amepoteza ‘mechi’ mbili lakini hiyo haiwapi nafasi ya kwenda bila kujiandaa kwani ‘timu’ hiyo ni kama mnyama mkali aliyesinzia na huwezi jua ataamka saa ngapi na ataamkia kwa nani.

Hivyo wanapaswa kujiandaa kwa ajili ya wapinzani wao kwa dhumuni la kuondoka na ushindi na kuongeza point katika mashindano hayo.

Simba iliyo nafasi ya tatu kwenye kundi B, inatarajia kuwa uwanjani siku ya Jumamosi  Desemba 9, kwenye mchezo wa tatu wa awamu ya kwanza ya hatua ya makundi dhidi ya Wydad ya Morocco.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags