Afariki kwa kudondokewa na jiwe, Mwanza

Afariki kwa kudondokewa na jiwe, Mwanza

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema mtu mmoja amefariki dunia baada ya kuangukiwa na jiwe akiwa katika shughuli za uchimbaji mawe.


Kwa mujibu wa Kamanda Katembo, tukio hilo limetokea Juni 26, 2023 saa 9 alasiri kwenye Kitongoji cha Mbulu, Kata ya Mayanga wilayani Mtwara na kwamba aliyefariki amefahamika kwa jina la Said Hassan Nampali (60).

“Siku ya tukio marehemu akiwa katika shughuli zake za kawaida za kuchimba mawe kwa ajili ya kuponda kokoto, ghafla jiwe hilo kubwa liliangula na kumkandamiza ambapo majirani baada ya kusikia kishindo kikubwa walisogea eneo hilo na kubaini uwepo mtu chini ya jiwe hilo,” amesema na kuongeza;

“Juhudi zilifanyika kwa kushirikiana na wananchi na mwili uliondolewa eneo la tukio na kupelekwa katika kituo cha afya Mikindani ambapo uchunguzi wa kitabibu umebaini chanzo cha kifo hicho kuwa ni kuangukiwa na jiwe hilo.”

Hivyo Kamanda Katembo ametahadharisha: “Natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuchukua tahadhari wanapokuwa wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia usalama kwanza ili kuepusha ajali zinazogharimu maisha ya watu.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags