Afanyiwa surgery mara 43 ili afanane na Barbie Dolls

Afanyiwa surgery mara 43 ili afanane na Barbie Dolls

Haya sasa kumekucha na mambo ya upasuaji (surgery) imefikia watu wanataka kuwa kama midol balaa jingine limetokea huko nchini Iraq mtangazaji na mwigizaji maarufu Dalia Naeem mwenye umri wa miaka 29.

Amefanyiwa upasuaji mara 43 ili kubadilisha muonekano wake afanane na Barbie Dolls.

Dalia ametumia maelfu ya dola za Kimarekani kuwa na muonekano huo,
Kutokana na mabadiliko hayo watu wengi wamejitokeza mitandaoni kumfatilia mpaka sasa amerekebishwa pua, masikio, ngozi ya uso imevutwa, midomo imejazwa, mashavu yamejazwa na kuongezwa matiti.

Japo kumekuwa na wahanga wengi wa upasuaji ila imeonyesha watu kuto hofia kupata madhara wakati mwengine mpaka kifo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags