Adidas mbioni kuzindua viatu vya Bob Marley

Adidas mbioni kuzindua viatu vya Bob Marley

Kampuni maarufu inayojihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ya Adidas iko mbioni kuzindua toleo maalumu la viatu vya marehemu mkali wa reggae kutoka Jamaica Bob Marley vijulikanavyo kama ‘retro SL 72’.

Ushirikiano huu unakuja baada ya historia ya ushirikiano wa Marley na Adidas, ikiwa ni pamoja na mwanamuziki huyo hapo awali alikuwa akipendelea kuvalia bidhaa za chapa hiyo.

Sneakers, hizo zinajumuisha picha na saini ya Bob Marley, zitakuwa sehemu ya bidhaa za Adidas ambapo zinatarajiwa kuingia sokoni majira ya joto 2024.



Ikumbukwe kuwa Marehemu Bob Marley alifariki katika Hospitali ya Jackson Memorial, Miami, Marekani Mei 11, mwaka 1981 akiwa na umri wa miaka 36 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags