Adele atangaza kufunga ndoa na Rich Paul

Adele atangaza kufunga ndoa na Rich Paul

Mwanamuziki Adele ametangaza kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu wakala wa wachezaji Marekani Rich Paul, ndoa inayotarajiwa kufungwa siku zijazo.

Adele amelithibitisha hilo siku ya jana Agosti 9 kwenye tamasha lake lililofanya nchini Ujerumani baada ya kusoma bango la shabiki lililokuwa limeandikwa ‘Will you marry me’ na kujibu kuwa hawezi.

“Siwezi kuoana na wewe, kwa sababu tayari ninaolewa” Mshindi huyo mara 16 wa Grammy alijibu huku akiinua mkono wake wa kushoto akioneshwa pete aliyovalishwa na Rich Paul.

Kwa miezi kadhaa Adele alikuwa akijiita mke wa Rich kwenye baadhi za posti zake hivyo basi huenda wawili hao wameamua kufanya kweli huku wakidaiwa kuwa muda wowote kuanzia sasa wanatarajia kuanzisha familia yaani kuwa na watoto.

Uhusiano wa Adele na Paul ulianza mwanzoni mwa mwaka 2021, ambapo walikutana kwa mara ya kwanza kwenye maonesho ya Vogue.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags