Adele achukizwa walinzi kuzuia shabiki asicheze, Ataka wamuache afurahi

Adele achukizwa walinzi kuzuia shabiki asicheze, Ataka wamuache afurahi

Mwanamuziki mkongwe Adele ameonesha kutofurahishwa na walinzi wa ukumbi wa The Colosseum katika Caesars Palace,  Las Vegas alipokuwa akitumbuiza baada ya walinzi hao kuonekana kila muda wakimkataza shabiki aliyefika kwenye onyesho hilo kusimama kwa kushangilia wakati, Adele aki-perform.

Walinzi walionekana kumsumbua shabiki huyo kwa kumkataza kila muda asisimame alipojaribu kutaka kufurahi pamoja na msanii huyo mbaye alikuwa akitumbuiza jukwaani.

Kutokana na hilo Adele aliona tukio hilo na kuwataka walinzi wamuache kijana huyo afurahi bila kusumbuliwa kwani amefika kwenye tamasha hilo kwa ajili ya kuburudika.

Kauli hiyo ya Adele iliibua hisia za mashabiki wengine katika ukumbi huo. walisikika wakipaza sauti kusema kuwa walinzi wanawakataza wasisimame, huku kijana aliyekuwa akisumbuliwa  naye akishindwa kujizuia hisia kutokana na kauli ya Adele kwa kuzidisha kupiga kelele.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags